SATURDAY APRIL 14 2018

London, England. Mashabiki wa Arsenal waamini kupangwa dhidi ya Atletico Madrid katika Europa Ligi itawapa ‘hukumu sahihi’ kwa sababu Arsene Wenger atatimuliwa wakitolewa au atabaki kwa kuwapa ubingwa na kupata tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao.
Mashabiki wa wengi wa Gunners waamini wapinzani wao ni kizingiti kikubwa kwao katika nusu fainali hiyo huku mechi nyingine itawakutanisha Marseille na Salzburg.
Baada ya kutazama ratiba hiyo, Mashabiki wengi wanaamini mambo mawili yatatoea kutwaa ubingwa Mei, au kuangalia Wenger akifungashiwa virago vyake na yote itategemea na matokeo ya mechi ya Atletico.
Atletico na Arsenal ndizo timu ambazo zimekuwa zikipewa nafasi kubwa ya kuchukua michuano hiyo, lakini sasa mmoja wao atakomea hatua ya nusu fainali.
Mashindano hayo ndiyo tiketi pekee ya uhakika kwa Arsenal kufuzu kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao baada ya kuwa nyuma kwa pointi 13 kwa timu inayoshika nafasi ya nne.
Kama Gunners itaifunga Atletico katika mechi hizo mbili, watakuwa wamejihakikishia kucheza fainali kwenye uwanja wa Parc Olympique Lyonnais jijini Lyon nchini Ufaransa.
No comments:
Post a Comment