Wednesday, April 18, 2018

fainali ya FA kupigwa sheikh amri abeid

Arusha waishukuru TFF fainali ya FA kupigwa Sheikh Amri Abeid

WEDNESDAY APRIL 18 2018


MWENYEKITI wa Chama Cha Soka Mkoa wa Arusha  (ARFA) Peter Temu amefurahishwa na maamuzi ya TFF  kuwaamini na kuwapatia nafasi ya kuwa wenyeji wa mashindano ya FA, yatakayofanyika Juni 2, mwaka huu kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
Temu amesema, tayari maandalizi ya fainali hizo zimeanza hasa kwenye suala la uwanja na ni bahati isiyoelezeka kupata nafasi hiyo kwa kuwa itawapatia fulsa wapenzi wa soka kupata kuwaona nyota wanaokipiga  ligi kuu na wajasiliamali kuongeza vipato.
“Uwanja wa Sheikh Amri Abeid ulifungwa kwa ajili ya ukarabati wa sehemu mbalimbali nadhani hilo ni moja ya viongozi wa soka kutupatia nafasi kwa kuwa siku nyingi viwanja ndio ilikuwa kikwazo kikubwa kupewa michezo,"anasema Temu.
“Muda mrefu timu za Ligi kuu hazijafika kucheza Arusha tangu JKT Oljoro ishuke daraja mwaka 2014 lakini mwaka jana Simba ilikuja kucheza na Madini Sc kwenye hatua ya robo fainali ya michuano hii na Yanga pia ilikuja kwa michezo ya kirafiki dhidi ya AFC.”
Aliongeza kuwa tayari viongozi wa TFF wamewasili mkoani hapa kukagua baadhi ya vitu ikiwemo uwanja na maeneo ya kufikia timu jambo ambalo Temu anaeleza halikumpatia hofu kwa kuwa Arusha imekamilika kila idara.
“Viongozi wa Serikali pamoja na wadau wa soka umefika muda wa kuungana kuhakikisha tunapata timu ya ligi kuu mwaka ujao maana hali hii inaleta aibu kubwa kwa Mkoa wetu uliokuwa unasifika kwa soka miaka ya nyuma,”anasema.
Msimamizi wa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Abdalah Kajembe amesema kwa sasa uwanja huo upo katika hali nzuri baada ya kufanyiwa ukarabati kwa zaidi ya miezi sita.

No comments:

Post a Comment