Friday, April 20, 2018

msukuma ataka wanasiasa washughulikiwe

Msukuma ataka wanasiasa Washughulikiwe....Asema Lema Saiv Kawa Binadamu Baada ya Kunyooshwa! 

Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Kasheku Musukuma amevitaka vyombo vya dola kuwashughulia watu wanaodaiwa kuwa wakorofi hasa wanasiasa, kwa kuwaweka ndani ili kurekebisha tabia zao.

Msukuma alitoa wito huo juzi Bungeni mjini Dodoma wakati akichangia hoja katika Wizara ya Katiba na Sheria.

“Sisi kama wabunge tunaotunga sheria tuviachie vyombo vifanye kazi yake, wanaosema kuna watu wamepotea hata watu wa CCM wamepotea wengi tu, wamechinjwa Kibiti wengi tu na hatukupiga kelele tumeviachia vyombo vinalishughulikia. 

"Hata mimi nilifanya kosa na niliwekwa ndani. Hawa wakorofi wakifanya makosa wawekwe magereza, unamuona Lema sasa hivi kidogo amekuwa binadamu,” alisema.

Aidha, Msukuma alimuomba Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi kupeleka bungeni muswada wa kubadilisha sheria ili makosa yasiyo stahili mtuhumiwa kufungwa apewe adhabu ndogo ili kuondoa msongamano wa wafungwa magerezani. 

harusi ya kiba

Harusi ya Alikiba Ukumbi/Mapambo Yagharimu sh milioni 40 za Tanzania

Mwandishi wetu aliyepo Mombasa, Mohammed Ahmed anaripoti kuwa mapambo katika ukumbi uliofanyika sherehe hiyo yamegharimu Sh2 milioni za Kenya ambazo ni wastani wa Sh40 milioni za Tanzania.

Mpambaji wa ukumbi wa Diamond Jubilee unaochukua watu 1,500 katika jiji hilo ambaye mwandishi wetu alimkuta akiendelea na kazi, anasema amelipwa kiasi hicho cha fedha ambacho ni kikubwa kulingana na aina ya mapambo waliochagua maharusi.


Inaelezwa kuwa familia ya binti huyo ina uhusiano wa karibu na Gavana wa Mombasa, Hassan Joho ambaye ni rafiki wa Alikiba.

Inaaminika kuwa Joho ndio amesaidia kwa kiasi kikubwa kumuunganisha Kiba na familia ya Amina, ambapo safari zake za mara kwa mara mjini Mombasa, hazikuwa kwa shughuli za kimuziki tu bali ni kuwa karibu na mkewe huyo mtarajiwa.

Harusi hiyo imefanyika jana Mombasa ambako Joho na vigogo wengine wa Muungano wa NASA walihudhuria  

Thursday, April 19, 2018

Bunge la Kenya kujadili umri wa mgombea urais

Bunge kujadili umri wa mgombea urais Kenya



Nairobi, Kenya. Bunge la Kenya limesema litashughulikia pendekezo la kuzuia mtu yeyote mwenye umri wa miaka 70 na zaidi kuwania urais na nyadhifa nyingine za kisiasa nchini humo.
Spika Justin Muturi amesema ameiamuru Kamati ya Bunge kuhusu Haki na Masuala ya Sheria (JLAC) kuchambua ombi hilo na kuwasilisha ripoti bungeni baada ya siku 60.
Ombi hilo liliwasilishwa na Mohamed Mohamud, mkazi wa Garissa ambaye anataka Bunge liifanyie mabadiliko Katiba ili kudhibiti umri wa wagombea mbalimbali wa nyadhifa za kisiasa.
Kwa mujibu wa Mohamud, siyo haki kwa watumishi wa umma kushinikizwa kustaafu wanapofikisha umri fulani, ikiwa wanasiasa wanaotaka kuwania nyadhifa katika chaguzi hawajadhibitiwa kiumri.
Amesema  mwenendo huu unawafanya viongozi wakongwe kukataa kuondoka katika ulingo wa siasa, "ili kutoa nafasi kwa kizazi cha wanasiasa wenye umri mdogo."
Mohamud  amesema  mtu mwenye umri wa miaka 70 hawezi kutekeleza  majukumu ya uongozi ipasavyo.
Hata hivyo, wabunge wa Jubilee na Nasa walipuuza pendekezo hilo wakisema kulishughulikia ni sawa na kulipotezea Bunge muda wake.
Baadhi yao wamesema  pendekezo hilo ni sehemu ya mkakati wa kumzuia kiongozi wa upinzani Raila Odinga kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa 2022.
Mbunge Robert Pukose alisema ombi hilo litaharibu mandhari ya siasa nchini hasa baada ya Odinga kuamua kushirikiana na Rais Uhuru Kenyatta.
"Pendekezo hili linapoteza muda  wa bunge na halingekubaliwa. Lina malengo mabaya na linafaa kukataliwa. Tunapaswa kuunda sheria kwa manufaa ya vizazi vijavyo hatutakiwi kuunda sheria zinazolenga watu fulani," alisema Dk Pukose ambaye ni mbunge wa Jubilee.
Naye Mbunge wa Mvita, Abdulswamad Nassir alisema pendekezo hilo linafaa kupewa muda mchache zaidi kwa sababu "halina maana yoyote."
"Mtu akiwasilisha ombi kama hili bunge, kamati husika inafaa kulipa muda wa dakika tatu pekee. Hii itazuia watu wengine kuwasilisha maombi mengine yasiyo na maana bungeni," amesema Nassir ambaye ni mbunge wa ODM.
Kiongozi wa wengi bungeni, Aden Duale hata hivyo amesema kila Mkenya ana haki ya kuwasilisha ombi bungeni kuhusu suala lolote kama kipengele cha 118 cha Katiba kinavyopendekeza.
"Huenda ombi hili sio nzuri. Huenda halina mwelekeo lakini hatutakiwi kupuuza kwani wananchi wengine wataogopa kuwasilisha maombi bungeni siku nyingine,"
amesema Duale ambaye ni mbunge wa Garrisa Mjini.
Ametoa wito kwa kamati ya JLAC inayoongozwa na Mbunge wa Baringo Kaskazini, William Cheptumo kuandaa ripoti ambayo itatoa mwelekeo kuhusu maombi kama hayo siku zijazo.
Licha ya kusema kuwa anashukuru malengo ya ombi hilo, kiongozi wa wachache bungeni, John Mbadi aliwaomba wabunge wengine kumpa nafasi Mohamud ya kusikilizwa na kujieleza.
"Tumpe muda. Huenda ana shida fulani na wazee. Kamati hiyo inatakiwa kumpa ushauri nasaha ili aweze kutambua kuwa hekima huja na umri," alisema Mbadi ambaye ni mbunge wa Suba Kusini.
Aliongeza kuwa marais wa zamani, Jomo Kenyatta na Mwai Kibaki waliingia madarakani wakiwa na umri wa zaidi ya miaka 70.
"Lakini licha ya kuwa na umri huo walitekeleza majukumu yao vizuri sawa na mwenzao Mzee Moi," alisema.
Mbunge wa Emurua, Dikirr Johanna Ng'eno ndiye pekee aliyeunga mkono pendekezo hilo la Mohamud.
"Huyu ni Mkenya jasiri ambaye anasema kile ambacho wengi wanaamini lakini wanaogopa kujitokeza hadharani," amesema  Ng'eno.
"Kuna baadhi ya watu ambao hutaka kubakia madarakani wakati ni wazi kuwa hawawezi kutekeleza wajibu wao ipasavyo kwa sababu ya kuwa na umri mkubwa. Mtindo huu sharti ukomeshwe."
Hata hivyo, Spika Muturi amewataka wabunge kutoa nafasi kwa kamati ya Cheptumo kushughulikia pendekezo hilo ipasavyo.
Naye Cheptumo amesema kwamba kamati yake itampa Mohamud muda wa kutosha ili aweze kuwasilisha hoja zake kwa njia huru.

mbeya city na chipukizi

Mbeya City yajikita kwa chipukizi

THURSDAY APRIL 19 2018


Dar es Salaam. Kocha wa Mbeya City, Ramadhan Nsanzurwimo amefichua sababu ya kutoa nafasi kwa kundi kubwa la wachezaji chipukizi katika dakika za lala salama za Ligi Kuu Bara kuwa ni kwa ajili ya kuwaandaa kuitumikia timu hiyo msimu ujao.
Nsazurwimo amesema kutokana na gharama kubwa ambazo timu zimekuwa zikipata katika kipindi cha dirisha la usajili, benchi lake la ufundi linaamini njia nzuri ya kuipunguzia timu mzigo ni kutengeneza wachezaji wake na si kusajili kutoka timu nyingine.
"Huwezi kujua kesho timu itakuwa kwenye hali gani kiuchumi kwani dirisha la usajili linaweza kufika na klabu ikawa haina hela ya kutosha kusajili ina maana ndio timu isiwe na wachezaji kwa ajili ya msimu ujao?  Ni lazima kama timu, iwe na vijana wake iliyowaibua na kuwaimarisha ili hata mambo ya kifedha yanaposumbua, tuwe na uhakika wa kuwa na wachezaji bora msimu ujao,"anasema Nsazurwimo.
Ndio maana kwa hizi mechi zilizosalia nimepanga kuwapa nafasi zaidi vijana wanaoonyesha kiwango bora ili waimarike na tuwapandishe moja kwa moja msimu ujao," alifafanua Nsanzurwimo.

Ngorongoro Heroes yaahidiwa zawadi nono

THURSDAY APRIL 19 2018


Dar es Salaam.Timu ya Taifa cha Vijana Tanzania chini ya miaka 20, Ngorongoro Heroes itaondoka kesho alfajiri kuelekea DR Congo tayari kwa mchezo wa marudiano dhidi ya wenyeji wao utakaopigwa Aprili 22.
Kocha Mkuu Ngorongoro Heroes, Ammy Ninje alisema wanatarajia kutoka na ushindi katika mchezo huo wa marudiano, baada ya kufanikiwa kurekebisha makosa waliyoyafanya katika mchezo wa kwanza.
“Mchezo huu una umuhimu kwetu kwahiyo tumefanya marekebisho mengi hasa katika upande wa ushambuliaji, tunaamini kabisa katika mchezo huu tutatoka na ushindi ili kuweza kusonga mbele zaidi,” alisema Ninje.
Wakati huo huo Hifadhi ya Ngorongoro Crater, imeidhamini safari ya timu hiyo kuelekea Congo, huku wakiweka wazi nia yao ya kuwa wadhamini wakuu katika timu hiyo.
 Kaimu Meneja Uhusiano wa Hifadhi hiyo, Joyce Mgaya alisema udhamini wao umetokana na uzalendo walionao huku wakiitaka timu hiyo kusonga mbele zaidi katika mashindano yao.
“Timu yetu ya Vijana inashiriki Mashindano makubwa kwa hiyo tutaitangaza hifadhi yetu, tumeanza kuidhamini safari yao kwenda Congo, lakini tunataka tuidhamini kabisa timu yetu hii ya Taifa, hivyo huu ni uzalendo mkubwa kwetu tuliouonyesha na kuitaka timu isonge mbele,” alisema.
Kocha Ninje alisema udhamini huo umewaongezea morali wachezaji wake kuelekea mechi yao ya marudiano dhidi ya Congo.
Ngorongoro wanatakiwa wapate ushindi katika mchezo wa marudiano dhidi ya Dr Congo baada ya mchezo wa awali kutoka sare ya bila kufungana, ili kuzidi kujihakikishia nafasi ya kufuzu kuelekea katika fainali za Afcon kwa timu za Vijana zitakazofanyika mwakani nchini Niger.

Bocco akubali yaishe kwa Okwi

THURSDAY APRIL 19 2018


Dar es Salaam. Simba sasa ni mwendo wa kukaba mpaka kivuli na ipo hivi, John Bocco hataki uchoyo kabisa, alipoona Emmanuel Okwi anaongoza kwa mabao ya kufunga, ameamua kumtengenezea njia ya kuhakikisha anatupia kila mechi.
Kati ya mambo anayoyafanya Bocco ni kumwachia Okwi apige faulo na penalti, wakati mwingine kumtengezea nafasi za kufunga anapomwona amekaa vizuri ndani ya 18, lengo anataka awe na idadi kubwa ya mabao.
Bocco amesema, haoni sababu ya kufanya uchoyo pindi anapomwona Okwi yupo kwenye nafasi nzuri ya kufunga kwa sababu kila mtu yupo kwa ajili ya manufaa ya Simba na si ya mtu binafsi.
"Okwi ndiye anayeongoza kwa mabao, lazima kama tuna namna yoyote ya kumwezesha tumpe ushirikiano ili tuweze kuandika rekodi ya aina yake msimu huu.
"Sina maana kwamba ninapopata nafasi ya kufunga nitajibweteka, napambana lakini lengo ni kutwaa ubingwa ambao unasubiriwa kwa hamu na mashabiki wetu," anasema Bocco ambaye amefunga mabao 14.
Bocco anasema kitu pekee anachokiona kitawawezesha kufikia malengo ni ushirikiano wa hali na mali na kujua wapo kwa ajili ya timu: "Sichezi ili mimi nionekane bora kuliko mwingine isipokuwa natimiza kile kilichonileta Simba na ndivyo ilivyo kila mchezaji anatakiwa kuwa hivyo,"anaeleza.
WENGINE WAMTAJA
Wakati huo huo; Kocha msaidizi wa Majimaji ya Songea, Habibu Kondo amemtaja Okwi wa Simba kuwa mchezaji hatari wa kuzifuma nyavu hasa watakapokutana mechi ya mzunguko wa pili baada ya raundi ya kwanza kufungwa mabao 4-0.
"Okwi ni mchezaji anayefunga kwa mahesabu na kuwahadaa mabeki, lazima aangaliwe kwa jicho la tofauti siku tutakapocheza nao mechi," anasema Kondo.
Kocha wa Ndanda FC, Malale Hamsini anasema kikosi kizima cha Simba kipo moto, lakini Okwi amemwona ana mipango ya kuzisakama nyavu za wapinzani, hivyo ni mchezaji  atakayetazamwa kwa jicho la ndani katika mechi yao.
"Ligi ni ngumu ni afadhari ucheze na Simba na Yanga kwa sasa, kuliko tukakutana wenyewe, lakini kuhusu Okwi ni mchezaji mzoefu ambaye anajua nini anataka katika ligi," alisema Malale.

Kiiza anarudi kucheza Bongo

THURSDAY APRIL 19 2018


Dar es Salaam. INASEMEKANA msimu ujao, mshambuliaji wa zamani wa Yanga na Simba, Hamis Kiiza ‘Diego’ anaweza akaonekana kwenye Ligi Kuu Bara, ingawa haijajulikana atavaa uzi wa timu gani.
Kiiza amekaririwa akisema anazungumza na timu mbalimbali za Bongo na kwamba kuna uwezekano mkubwa wa kurejea kucheza ligi ya Tanzania anayoifuatilia kwa ukaribu ili kujua kinachoendelea.
"Ligi ya Bongo ina ushindani wa hali ya juu, ninazungumza na timu mbalimbali ingawa siwezi kuziweka wazi kwa sasa, mambo yakienda sawa itajulikana naamini bado nitaonyesha uwezo wa hali ya juu, siri ni kujituma na kujitambua basi," alisema Mganda huyo.
Kiiza kwa sasa anacheza soka la kulipwa Sudan katika klabu ya Al-Hilal SC inayoshiriki Ligi Kuu ya nchini humo.

Lipuli yatangaza vita dhidi ya si

Lipuli yaitangazia vita Simba

THURSDAY APRIL 19 2018
 

Iringa. Lipuli FC imesema itaingia uwanjani kwa lengo kuweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza kuifunga Simba msimu huu wakati wataposhuka kwenye Uwanja wa Samora, Iringa Jumamosi hii.
Mchezo huo wa ligi awali ulikuwa uchezwe kesho Aprili 20, lakini kutokana na wammiliki wa uwanja kuwa na matumizi nao imesababisha mechi hiyo kusogezwa mbele hadi Aprili 21 Jumamosi umewaweka mashabiki wa timu zote mbili kuwa katika hali ya kuusubiri kwa hamu kubwa kufuatia matokeo ya mchezo wa awali kumalizika kwa sare 1-1 zilipokutana jijini Dar Es Salaam.
Akizungumza mchezo huo leo asubuhi, Kocha Msaidizi wa Lipuli Fc, Seleman Matola amesema maandalizi yote yamekamilika na kuahidi kuwafunga vinara hao wa ligi Simba Sc katika mchezo huo.
“Namshukuru Mwenyezi Mungu kikosi changu kiko salama maandalizi yamekuwa ni mazuri wachezaji wamejiandaa kwa ajili ya mchezo wa Jumamosi, samba ni timu kubwa timu ngumu timu ambayo imewekeza katika mpira ambayo imefanya vizuri katika msimu huu,” alisema Matola.
Matola aliongeza “Simba haijafungwa sisi tunataka tujiandae tuwe timu ya kwanza kumchinja mnyama katika uwanja wa nyumbani kwa hiyo maandalizi ya kupata pointi tatu yanaenda vizuri kabisa.”
Lipuli Fc kwa sasa ipo nafasi ya 8 katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 31, wakati Simba inaongoza Ligi Kuu ikiwa na pointi 58.

Wednesday, April 18, 2018

Mashabiki wa Arsenal wagoma kwenda Uwanjani

TUESDAY APRIL 17 2018

London, England. Idadi ndogo ya mashabiki waliojitokeza katika mchezo wa Ligi Kuu England kati ya Arsenal dhidi ya Newcastle United, unaweza kumng’oa kocha Arsene Wenger.
Baadhi ya viti vya Uwanja wa Emirates vilibaki wazi baada ya mashabiki wa Arsenal kususa.
Kipigo cha mabao 2-1 ilichopata kutoka kwa Newcastle, kinamuweka katika mazingira magumu kocha huyo aliyeanza kuinoa Arsenal tangu mwaka 1996.
Mashabiki wa klabu hiyo kwa takribani mechi nne za ligi ilizocheza Arsenal walikuwa wachache uamuzi unaoweza kumgharimu Wenger majira ya kiangazi.
Licha ya kuendelea kupambana katika Kombe la Europa, Arsenal imejiweka katika nafasi ndogo ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya mwakani.


mohamed salah anastahiri kuwa mwanasoka bora england 2018


SALUTI Shearer adai Salah mwanasoka bora England

TUESDAY APRIL 17 2018

MANCHESTER ENGLAND
MAMBO ya ubingwa yameisha. Sasa hivi kuna mbio nyingine za kimya kimya. Nani anastahili kuwa mwanasoka bora wa msimu huu? kuna wanaosema Kevin De Bruyne wa Manchester City, halafu kuna wanaosema Mohamed Salah wa Liverpool.
Alan Shearer, staa wa zamani wa Blackburn, Newcastle United na timu ya taifa ya England anaamini kwamba staa wa Liverpool, Mohamed Salah anastahili kuwa mwanasoka mwanasoka bora wa msimu huu Ligi Kuu ya England.
Salah mpaka sasa anaongoza kwa kufunga mabao katika Ligi Kuu ya England akiwa amefikisha mabao 30 huku kwa ujumla akiwa amefunga mabao 40 katika michuano mbalimbali msimu huu. shearer anaamini kwa dhati kwamba De Bruyne amefanya makubwa lakini Salah anatisha.
“Kwa Mo salah kufunga mabao 30 katika msimu wake wa kwanza Liverpool ni mafanikio ya ajabu. Ni mchezaji wa nane katika historia ya Ligi Kuu ya England kufikia idadi hiyo, katika orodha ambayo mimi mwenyewe pia nipo.” Alisema Shearer.
“Na Salah amefanya hayo akiwa sio mshambuliaji wa kati moja kwa moja kama nilivyokuwa mimi au mpinzani wake katika kiatu cha dhahabu, Harry Kane. Ni kitu kizuri ukijua kwamba unakwenda uwanjani na utafunga bao. Sio mara nyingi katika maisha yako ya soka utajisikia hivyo.” Aliongeza mkongwe huyo.
“Kwa fomu ambayo anayo sasa, ndivyo ambavyo Salah anajisikia kila wakati anaposimama katika mlango wa kuingilia uwanjani kabla ya mechi. Hakuna ambaye alitazamia kama angekuwa moto wakati ananunuliwa na Liverpool katika dirisha kubwa lililopita.” Aliongeza Shearer.
“Kw akweli kulikuwa na wasiwasi wakati Liverpool ilipolipa kiasi cha pauni 34 milioni kwa ajili yake, hasa kwa namna jinsi kipindi chake kwa Chelsea kilivyokwenda. Kwa sasa anapata kura yangu ya kuwa mchezaji bora wa mwaka.”
“Nilisema ningesubiri kuona mechi ya Liverpool ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya dhidi ya Manchester City ambavyo ingekwenda kabla ya kuamua nani anastahili tuzo kati ya Salah au Kevin De Bruyne. Lakini kwa Salah kufunga mechi zote hizo mbili na kuipeleka timu nusu fainali kwa sasa namchagua yeye.”
“De Bruyne amekuwa bora sana na kwa mara nyingine alikuwa bora Jumamosi dhidi ya Tottenham. Lakini nafahamu kuna ugumu gani katika kufunga mabao na ndio maana ningempa kura yangu Salah ambaye kwa sasa ana mabao 40 katika michuano yote Liverpool.”
Kauli ya Shearer ni mwendelezo tu. tayari mpinzani wa Salah, De Bruyne amekiri kwamba staa huyo wa kimataifa wa Misri anastaili kuteulizwa kuwa mwanasoka bora wa England mbele yake.
“Nadhani kama hautamchagua yeyote kutoka katika timu yetu basi yeye anastahili. Nadhani ataenda kutwaa kwa namna yoyote ile. Amekuwa mkali sana na kushindana na mtu ambaye anafunga mabao mengi ni vigumu sana kushinda. Nimeridhishwa na kiwango changu cha msimu huu, pamoja na kiwango cha timu.” Alisema De Bruyne.
Kwa vile wachezaji wa timu moja hawaruhusiwi kupigiana kura, De Bruyne anadia kwamba kama angeweza kufanya hivyo basi kura yake ingeenda kwa kiungo mwenzake wa Manchester City, David Silva.
“Kwangu mimi, kama ningeweza kupiga kura kama ningempigia David Silva. Jinsi alivyokuwa katika matatizo na mwanae na siku zote amekuwa akisafiri, bila ya mazoezi, lakini kwa jinsi alivyocheza, amekuwa bora sana. lakini Salah anastahili pia kwa kweli.”

Kabange amshangaa Okwi

WEDNESDAY APRIL 18 2018


KOCHA msaidizi wa Njombe Mji, Mlage Kabange amesema  Emmanuel Okwi wa Simba ni mjanja kwa Ligi Kuu  Bara, lakini akienda nje makali yake hayaonekani.
Kabange anasema Okwi alipata dili la kucheza soka la kulipwa nchini, Denmark katika klabu ya  Sønderjyske, lakini alishindwa kuwika kama anavyofanya katika ligi ya Tanzania.
"Kwa ligi ya Tanzania, kusema ukweli Okwi amejua kuwakimbiza na kuwanyamazisha wale waliokuwa wanamwita mhenga, jina hilo kwa sasa limefutika, ajabu akienda nje mbona haonyeshi makali!" amehoji Kabange.
Alienda mbali na kuwataka wachezaji wanaocheza ligi kuu, kushtuka na kujifunza kwa mastaa wa nje kama Okwi, kujua kwa nini kila anakuja nchini anawafunika ndipo wanapoweza kupiga hatua.
"Tatizo kwa wachezaji wetu sio wale ambao wanapenda kujifunza kwa mwingine, wakijihoji watajua jinsi ya kuonyesha ushindani dhidi yake ama mfano wa kiungo wa Yanga, Tshishimbi waangalie ana vitu gani ambavyo wao hawana, lakini utakuwa wanaleta dharau,"anasema.