Wednesday, April 18, 2018

mohamed salah anastahiri kuwa mwanasoka bora england 2018


SALUTI Shearer adai Salah mwanasoka bora England

TUESDAY APRIL 17 2018

MANCHESTER ENGLAND
MAMBO ya ubingwa yameisha. Sasa hivi kuna mbio nyingine za kimya kimya. Nani anastahili kuwa mwanasoka bora wa msimu huu? kuna wanaosema Kevin De Bruyne wa Manchester City, halafu kuna wanaosema Mohamed Salah wa Liverpool.
Alan Shearer, staa wa zamani wa Blackburn, Newcastle United na timu ya taifa ya England anaamini kwamba staa wa Liverpool, Mohamed Salah anastahili kuwa mwanasoka mwanasoka bora wa msimu huu Ligi Kuu ya England.
Salah mpaka sasa anaongoza kwa kufunga mabao katika Ligi Kuu ya England akiwa amefikisha mabao 30 huku kwa ujumla akiwa amefunga mabao 40 katika michuano mbalimbali msimu huu. shearer anaamini kwa dhati kwamba De Bruyne amefanya makubwa lakini Salah anatisha.
“Kwa Mo salah kufunga mabao 30 katika msimu wake wa kwanza Liverpool ni mafanikio ya ajabu. Ni mchezaji wa nane katika historia ya Ligi Kuu ya England kufikia idadi hiyo, katika orodha ambayo mimi mwenyewe pia nipo.” Alisema Shearer.
“Na Salah amefanya hayo akiwa sio mshambuliaji wa kati moja kwa moja kama nilivyokuwa mimi au mpinzani wake katika kiatu cha dhahabu, Harry Kane. Ni kitu kizuri ukijua kwamba unakwenda uwanjani na utafunga bao. Sio mara nyingi katika maisha yako ya soka utajisikia hivyo.” Aliongeza mkongwe huyo.
“Kwa fomu ambayo anayo sasa, ndivyo ambavyo Salah anajisikia kila wakati anaposimama katika mlango wa kuingilia uwanjani kabla ya mechi. Hakuna ambaye alitazamia kama angekuwa moto wakati ananunuliwa na Liverpool katika dirisha kubwa lililopita.” Aliongeza Shearer.
“Kw akweli kulikuwa na wasiwasi wakati Liverpool ilipolipa kiasi cha pauni 34 milioni kwa ajili yake, hasa kwa namna jinsi kipindi chake kwa Chelsea kilivyokwenda. Kwa sasa anapata kura yangu ya kuwa mchezaji bora wa mwaka.”
“Nilisema ningesubiri kuona mechi ya Liverpool ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya dhidi ya Manchester City ambavyo ingekwenda kabla ya kuamua nani anastahili tuzo kati ya Salah au Kevin De Bruyne. Lakini kwa Salah kufunga mechi zote hizo mbili na kuipeleka timu nusu fainali kwa sasa namchagua yeye.”
“De Bruyne amekuwa bora sana na kwa mara nyingine alikuwa bora Jumamosi dhidi ya Tottenham. Lakini nafahamu kuna ugumu gani katika kufunga mabao na ndio maana ningempa kura yangu Salah ambaye kwa sasa ana mabao 40 katika michuano yote Liverpool.”
Kauli ya Shearer ni mwendelezo tu. tayari mpinzani wa Salah, De Bruyne amekiri kwamba staa huyo wa kimataifa wa Misri anastaili kuteulizwa kuwa mwanasoka bora wa England mbele yake.
“Nadhani kama hautamchagua yeyote kutoka katika timu yetu basi yeye anastahili. Nadhani ataenda kutwaa kwa namna yoyote ile. Amekuwa mkali sana na kushindana na mtu ambaye anafunga mabao mengi ni vigumu sana kushinda. Nimeridhishwa na kiwango changu cha msimu huu, pamoja na kiwango cha timu.” Alisema De Bruyne.
Kwa vile wachezaji wa timu moja hawaruhusiwi kupigiana kura, De Bruyne anadia kwamba kama angeweza kufanya hivyo basi kura yake ingeenda kwa kiungo mwenzake wa Manchester City, David Silva.
“Kwangu mimi, kama ningeweza kupiga kura kama ningempigia David Silva. Jinsi alivyokuwa katika matatizo na mwanae na siku zote amekuwa akisafiri, bila ya mazoezi, lakini kwa jinsi alivyocheza, amekuwa bora sana. lakini Salah anastahili pia kwa kweli.”

No comments:

Post a Comment