Wednesday, April 18, 2018

Kabange amshangaa Okwi

WEDNESDAY APRIL 18 2018


KOCHA msaidizi wa Njombe Mji, Mlage Kabange amesema  Emmanuel Okwi wa Simba ni mjanja kwa Ligi Kuu  Bara, lakini akienda nje makali yake hayaonekani.
Kabange anasema Okwi alipata dili la kucheza soka la kulipwa nchini, Denmark katika klabu ya  Sønderjyske, lakini alishindwa kuwika kama anavyofanya katika ligi ya Tanzania.
"Kwa ligi ya Tanzania, kusema ukweli Okwi amejua kuwakimbiza na kuwanyamazisha wale waliokuwa wanamwita mhenga, jina hilo kwa sasa limefutika, ajabu akienda nje mbona haonyeshi makali!" amehoji Kabange.
Alienda mbali na kuwataka wachezaji wanaocheza ligi kuu, kushtuka na kujifunza kwa mastaa wa nje kama Okwi, kujua kwa nini kila anakuja nchini anawafunika ndipo wanapoweza kupiga hatua.
"Tatizo kwa wachezaji wetu sio wale ambao wanapenda kujifunza kwa mwingine, wakijihoji watajua jinsi ya kuonyesha ushindani dhidi yake ama mfano wa kiungo wa Yanga, Tshishimbi waangalie ana vitu gani ambavyo wao hawana, lakini utakuwa wanaleta dharau,"anasema.

No comments:

Post a Comment